Yeremia 23:18
Jeremiah 23:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini ni yupi miongoni mwao aliyesimama katika baraza la Bwana ili kuona au kusikia neno lake? Ni nani aliyesikiliza na kusikia neno lake?
Jeremiah 23:18 in English
Jeremiah 23:18 · Berean Standard Bible
But which of them has stood in the council of the LORD to see and hear His word? Who has given heed to His word and obeyed it?
Context
16Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo:
“Msisikilize wanachowatabiria manabii,
wanawajaza matumaini ya uongo.
Wanasema maono kutoka akili zao wenyewe,
hayatoki katika kinywa cha Bwana. 17Huendelea kuwaambia wale wanaonidharau mimi,
‘Bwana asema: Mtakuwa na amani.’
Kwa wale wote wafuatao ugumu wa mioyo yao,
wao husema, ‘Hakuna dhara litakalowapata.’ 18Lakini ni yupi miongoni mwao aliyesimama katika baraza la Bwana
ili kuona au kusikia neno lake?
Ni nani aliyesikiliza
na kusikia neno lake? 19Tazama, dhoruba ya Bwana
itapasuka kwa ghadhabu,
kisulisuli kitazunguka na kuanguka
vichwani vya waovu. 20Hasira ya Bwana haitageuka mpaka amelitimiza kusudi la moyo wake.
Siku zijazo mtalifahamu kwa wazi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.