Yeremia 22:16
Jeremiah 22:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Aliwatetea maskini na wahitaji, hivyo yeye akafanikiwa katika yote. Je, hiyo si ndiyo maana ya kunijua mimi?” asema Bwana.
Jeremiah 22:16 in English
Jeremiah 22:16 · Berean Standard Bible
He took up the cause of the poor and needy, and so it went well with him. Is this not what it means to know Me?” declares the LORD.
Context
14Asema, ‘Nitajijengea jumba kuu la kifalme,
na vyumba vya juu vyenye nafasi kubwa.’
Hivyo anaweka ndani yake madirisha makubwa,
huweka kuta za mbao za mierezi,
na kuipamba kwa rangi nyekundu. 15“Je, inakufanya kuwa mfalme
huko kuongeza idadi ya mierezi?
Je, baba yako hakuwa na chakula na kinywaji?
Alifanya yaliyo sawa na haki,
hivyo yeye akafanikiwa katika yote. 16Aliwatetea maskini na wahitaji,
hivyo yeye akafanikiwa katika yote.
Je, hiyo si ndiyo maana ya kunijua mimi?”
asema Bwana. 17“Lakini macho yako na moyo wako vimeelekezwa tu
katika mapato ya udhalimu,
kwa kumwaga damu isiyo na hatia,
kwa uonevu na ukatili.” 18Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana kuhusu Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda:
“Hawatamwombolezea wakisema:
‘Ole, ndugu yangu! Ole, umbu langu!’
Hawatamwombolezea wakisema:
‘Ole, bwana wangu! Ole, fahari yake!’
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.