Yeremia 13:26
Jeremiah 13:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nitayafunua marinda yako mpaka juu ya uso wako ili aibu yako ionekane:
Jeremiah 13:26 in English
Jeremiah 13:26 · Berean Standard Bible
So I will pull your skirts up over your face, that your shame may be seen.
Context
24“Nitawatawanya kama makapi
yapeperushwayo na upepo wa jangwani. 25Hii ndiyo kura yako,
fungu nililokuamuria,”
asema Bwana,
“kwa sababu umenisahau mimi
na kuamini miungu ya uongo. 26Nitayafunua marinda yako mpaka juu ya uso wako
ili aibu yako ionekane: 27uzinzi wako na kulia kwako kama farasi kulikojaa tamaa,
ukahaba wako usio na aibu!
Nimeyaona matendo yako ya machukizo
juu ya vilima na mashambani.
Ole wako, ee Yerusalemu!
Utaendelea kuwa najisi mpaka lini?”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.