Yeremia 13:24
Jeremiah 13:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Nitawatawanya kama makapi yapeperushwayo na upepo wa jangwani.
Jeremiah 13:24 in English
Jeremiah 13:24 · Berean Standard Bible
“I will scatter you like chaff driven by the desert wind.
Context
22Nawe kama ukijiuliza,
“Kwa nini haya yamenitokea?”
Ni kwa sababu ya dhambi zako nyingi
ndipo marinda yako yameraruliwa
na mwili wako umetendewa vibaya. 23Je, Mkushi aweza kubadili ngozi yake
au chui kubadili madoadoa yake?
Vivyo hivyo nawe huwezi kufanya mema
wewe uliyezoea kutenda mabaya. 24“Nitawatawanya kama makapi
yapeperushwayo na upepo wa jangwani. 25Hii ndiyo kura yako,
fungu nililokuamuria,”
asema Bwana,
“kwa sababu umenisahau mimi
na kuamini miungu ya uongo. 26Nitayafunua marinda yako mpaka juu ya uso wako
ili aibu yako ionekane:
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.