Yeremia 13:20
Jeremiah 13:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Inua macho yako uone wale wanaokuja kutoka kaskazini. Liko wapi lile kundi ulilokabidhiwa, kondoo wale uliojivunia?
Jeremiah 13:20 in English
Jeremiah 13:20 · Berean Standard Bible
Lift up your eyes and see those coming from the north. Where is the flock entrusted to you, the sheep that were your pride?
Context
18Mwambie mfalme na mamaye,
“Shukeni kutoka kwenye viti vyenu vya enzi,
kwa kuwa taji zenu za utukufu
zitaanguka kutoka vichwani mwenu.” 19Miji iliyoko Negebu itafungwa,
wala hapatakuwa na mtu wa kuifungua.
Watu wa Yuda wote watapelekwa uhamishoni,
wakichukuliwa kabisa waende mbali. 20Inua macho yako uone
wale wanaokuja kutoka kaskazini.
Liko wapi lile kundi ulilokabidhiwa,
kondoo wale uliojivunia? 21Utasema nini Bwana atakapowaweka juu yako
wale ulioungana nao kama marafiki wako maalum?
Je, hutapatwa na utungu kama mwanamke
aliye katika utungu wa kuzaa? 22Nawe kama ukijiuliza,
“Kwa nini haya yamenitokea?”
Ni kwa sababu ya dhambi zako nyingi
ndipo marinda yako yameraruliwa
na mwili wako umetendewa vibaya.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.