Yeremia 13:15
Jeremiah 13:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Sikieni na mzingatie, msiwe na kiburi, kwa kuwa Bwana amenena.
Jeremiah 13:15 in English
Jeremiah 13:15 · Berean Standard Bible
Listen and give heed. Do not be arrogant, for the LORD has spoken.
Context
13Kisha uwaambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana: nitawajaza ulevi wote waishio katika nchi hii, pamoja na wafalme waketio juu ya kiti cha enzi cha Daudi, makuhani, manabii na wale wote waishio Yerusalemu. 14Nitawagonganisha kila mmoja na mwenzake, baba na wana wao, asema Bwana. Sitawarehemu wala kuwahurumia ili niache kuwaangamiza.’ ” 15Sikieni na mzingatie,
msiwe na kiburi,
kwa kuwa Bwana amenena. 16Mpeni utukufu Bwana Mungu wenu,
kabla hajaleta giza,
kabla miguu yenu haijajikwaa
juu ya vilima vitakavyotiwa giza.
Mlitarajia nuru,
lakini ataifanya kuwa giza nene
na kuibadili kuwa huzuni kubwa. 17Lakini kama hamtasikiliza,
nitalia sirini
kwa ajili ya kiburi chenu;
macho yangu yatalia kwa uchungu,
yakitiririka machozi,
kwa sababu kundi la kondoo la Bwana
litachukuliwa mateka.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.