Yeremia 11:14
Jeremiah 11:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Wewe usiwaombee watu hawa wala kufanya maombezi yoyote au kunisihi kwa ajili yao, kwa sababu sitawasikiliza watakaponiita wakati wa taabu yao.
Jeremiah 11:14 in English
Jeremiah 11:14 · Berean Standard Bible
As for you, do not pray for these people. Do not raise up a cry or a prayer on their behalf, for I will not be listening when they call out to Me in their time of disaster.
Context
12Miji ya Yuda na watu wa Yerusalemu watakwenda kuililia miungu ambayo wameifukizia uvumba, lakini haitawasaidia kamwe wakati maafa yatakapowapiga. 13Mnayo miungu mingi kama miji mliyo nayo, ee Yuda, nazo madhabahu mlizozijenga za kufukizia uvumba huyo mungu wa aibu Baali ni nyingi kama barabara za Yerusalemu.’ 14“Wewe usiwaombee watu hawa wala kufanya maombezi yoyote au kunisihi kwa ajili yao, kwa sababu sitawasikiliza watakaponiita wakati wa taabu yao. 15“Mpenzi wangu anafanya nini hekaluni mwangu,
anapofanya mashauri yake maovu na wengi?
Je, nyama iliyowekwa wakfu yaweza
kuondolea mbali adhabu yako?
Unapojiingiza katika ubaya wako,
ndipo unashangilia.” 16Bwana alikuita mti wa mzeituni uliostawi
ulio na matunda mazuri kwa sura.
Lakini kwa ngurumo ya mawimbi makuu
atautia moto,
nayo matawi yake yatavunjika.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.