Native Bible

Judges 9:55 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Waisraeli walipoona kuwa Abimeleki amekufa, kila mtu akaenda nyumbani kwake.

Judges 9:55 in English

Judges 9:55 · Berean Standard Bible

And when the Israelites saw that Abimelech was dead, they all went home.

Context

53mwanamke mmoja akaangusha sehemu ya juu ya jiwe la kusagia juu ya kichwa cha Abimeleki, likapasua fuvu la kichwa chake. 54Akamwita kwa haraka kijana yule aliyechukua silaha zake, na kumwambia, “Chukua upanga wako na uniue, watu wasije wakasema kwamba, ‘Mwanamke amemuua.’ ” Basi yule kijana akamchoma upanga, naye akafa. 55Waisraeli walipoona kuwa Abimeleki amekufa, kila mtu akaenda nyumbani kwake. 56Hivyo ndivyo Mungu alivyolipiza uovu ule ambao Abimeleki alikuwa ameutenda kwa baba yake kwa kuwaua ndugu zake sabini. 57Mungu akawapatiliza watu wa Shekemu uovu wao juu ya vichwa vyao, na juu yao ikaja laana ya Yothamu mwana wa Yerub-Baali.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.