Waamuzi 9:41
Judges 9:41 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Abimeleki akakaa Aruma, naye Zebuli akawafukuza Gaali na ndugu zake watoke Shekemu.
Judges 9:41 in English
Judges 9:41 · Berean Standard Bible
Abimelech stayed in Arumah, and Zebul drove Gaal and his brothers out of Shechem.
Context
39Basi Gaali akatoka akawaongoza watu wa Shekemu kupigana na Abimeleki. 40Abimeleki akamfukuza, watu wengi wakajeruhiwa katika kukimbia huko, njia nzima hadi kwenye ingilio la lango. 41Abimeleki akakaa Aruma, naye Zebuli akawafukuza Gaali na ndugu zake watoke Shekemu. 42Kesho yake watu wa Shekemu wakatoka wakaenda mashambani, Abimeleki akaambiwa juu ya jambo hili. 43Hivyo akawachukua watu wake, akawagawanya katika vikosi vitatu na kuwaweka waviziao huko mashambani. Alipowaona watu wanatoka kwenda nje ya mji, akainuka dhidi yao na kuwashambulia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.