Waamuzi 9:39
Judges 9:39 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Basi Gaali akatoka akawaongoza watu wa Shekemu kupigana na Abimeleki.
Judges 9:39 in English
Judges 9:39 · Berean Standard Bible
So Gaal went out before the leaders of Shechem and fought against Abimelech,
Context
37Lakini Gaali akasema tena, “Tazama, watu wanashuka kutoka katikati ya nchi na kikosi kimoja kinakuja kutoka Tabur-Ezeri na kikosi kingine kutoka upande wa Elon-Meonenimu.” 38Ndipo Zebuli akamwambia, “Kuko wapi kujivuna kwako sasa, wewe uliyesema, ‘Huyo Abimeleki ni nani hata tumtumikie?’ Hawa si wale watu uliowadharau? Toka nje sasa ukapigane nao!” 39Basi Gaali akatoka akawaongoza watu wa Shekemu kupigana na Abimeleki. 40Abimeleki akamfukuza, watu wengi wakajeruhiwa katika kukimbia huko, njia nzima hadi kwenye ingilio la lango. 41Abimeleki akakaa Aruma, naye Zebuli akawafukuza Gaali na ndugu zake watoke Shekemu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.