Waamuzi 9:37
Judges 9:37 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini Gaali akasema tena, “Tazama, watu wanashuka kutoka katikati ya nchi na kikosi kimoja kinakuja kutoka Tabur-Ezeri na kikosi kingine kutoka upande wa Elon-Meonenimu.”
Judges 9:37 in English
Judges 9:37 · Berean Standard Bible
Then Gaal spoke up again, “Look, people are coming down from the center of the land,* and one company is coming by way of the Diviners’ Oak.*”
Context
35Basi Gaali mwana wa Ebedi alikuwa ametoka nje akawa amesimama katika ingilio la mji wakati ule ule ambao Abimeleki na watu wake walipokuwa wanatoka sehemu zao za maficho. 36Gaali alipowaona, akamwambia Zebuli, “Tazama, watu wanashuka kutoka kwenye vilele vya milima!”
Zebuli akajibu, “Wewe unaona vivuli vya milima kana kwamba ni watu.” 37Lakini Gaali akasema tena, “Tazama, watu wanashuka kutoka katikati ya nchi na kikosi kimoja kinakuja kutoka Tabur-Ezeri na kikosi kingine kutoka upande wa Elon-Meonenimu.” 38Ndipo Zebuli akamwambia, “Kuko wapi kujivuna kwako sasa, wewe uliyesema, ‘Huyo Abimeleki ni nani hata tumtumikie?’ Hawa si wale watu uliowadharau? Toka nje sasa ukapigane nao!” 39Basi Gaali akatoka akawaongoza watu wa Shekemu kupigana na Abimeleki.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.