Waamuzi 6:7
Judges 6:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Waisraeli walipomlilia Bwana kwa sababu ya Wamidiani,
Judges 6:7 in English
Judges 6:7 · Berean Standard Bible
Now when the Israelites cried out to the LORD because of Midian,
Context
5Walipanda na mifugo yao na mahema yao, mfano wa makundi ya nzige. Ilikuwa haiwezekani kuwahesabu watu na ngamia zao; wakavamia nchi ili kuiharibu. 6Waisraeli wakafanywa kuwa maskini sana na Wamidiani, hata Israeli wakamlilia Bwana kuomba msaada. 7Waisraeli walipomlilia Bwana kwa sababu ya Wamidiani, 8Bwana akawapelekea nabii, ambaye aliwaambia, “Hili ndilo Bwana, Mungu wa Israeli, asemalo: Niliwapandisha mtoke Misri, toka nchi ya utumwa. 9Nikawanyakua kutoka mikononi mwa Wamisri na kutoka mikononi mwa watesi wenu wote. Nikawafukuza watoke mbele yenu nami nikawapa ninyi nchi yao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.