Waamuzi 5:9
Judges 5:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Moyo wangu u pamoja na wakuu wa Israeli, pamoja na wale wanaojitoa wenyewe kwa hiari yao miongoni mwa watu. Mhimidini Bwana!
Judges 5:9 in English
Judges 5:9 · Berean Standard Bible
My heart is with the princes of Israel, with the volunteers among the people. Bless the LORD!
Context
7Mashujaa walikoma katika Israeli,
walikoma mpaka mimi, Debora, nilipoinuka,
nilipoinuka kama mama katika Israeli. 8Walipochagua miungu migeni,
vita vilikuja katika malango ya mji,
hapakuonekana ngao wala mkuki
miongoni mwa mashujaa 40,000 katika Israeli. 9Moyo wangu u pamoja na wakuu wa Israeli,
pamoja na wale wanaojitoa wenyewe
kwa hiari yao miongoni mwa watu.
Mhimidini Bwana! 10“Nanyi mpandao punda weupe,
mkiketi juu ya matandiko ya thamani,
nanyi mtembeao barabarani,
fikirini 11juu ya sauti za waimbaji
mahali pa kunyweshea maji.
Wanasimulia matendo ya haki ya Bwana,
matendo ya haki ya mashujaa wake
katika Israeli.
“Ndipo watu wa Bwana
walipoteremka malangoni pa mji.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.