Waamuzi 5:6
Judges 5:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Katika siku za Shamgari mwana wa Anathi, katika siku za Yaeli, barabara kuu hazikuwa na watu; wasafiri walipita njia za kando.
Judges 5:6 in English
Judges 5:6 · Berean Standard Bible
In the days of Shamgar son of Anath, in the days of Jael, the highways were deserted and the travelers took the byways.
Context
4“Ee Bwana, ulipotoka katika Seiri,
ulipopita katika mashamba ya Edomu,
nchi ilitetemeka, mbingu nazo zikamwaga,
naam, mawingu yakamwaga maji. 5Milima ilitetemeka mbele za Bwana,
hata ule wa Sinai,
mbele za Bwana,
Mungu wa Israeli. 6“Katika siku za Shamgari mwana wa Anathi,
katika siku za Yaeli,
barabara kuu hazikuwa na watu;
wasafiri walipita njia za kando. 7Mashujaa walikoma katika Israeli,
walikoma mpaka mimi, Debora, nilipoinuka,
nilipoinuka kama mama katika Israeli. 8Walipochagua miungu migeni,
vita vilikuja katika malango ya mji,
hapakuonekana ngao wala mkuki
miongoni mwa mashujaa 40,000 katika Israeli.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.