Native Bible

Judges 5:29 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wanawake wenye busara kuliko wengine wote wakamjibu; naam, husema moyoni mwake,

Judges 5:29 in English

Judges 5:29 · Berean Standard Bible

Her wisest ladies answer; indeed she keeps telling herself,

Context

27Aliinama miguuni pa Yaeli, akaanguka; akalala hapo. Pale alipoinama miguuni pake, alianguka; pale alipoinamia, ndipo alipoanguka, akiwa amekufa. 28“Kupitia dirishani mamaye Sisera alichungulia; nyuma ya dirisha alilia, akasema, ‘Mbona gari lake linachelewa kufika? Mbona vishindo vya magari yake vimechelewa?’ 29Wanawake wenye busara kuliko wengine wote wakamjibu; naam, husema moyoni mwake, 30‘Je, hawapati na kugawanya nyara: msichana mmoja au wawili kwa kila mtu, mavazi ya rangi mbalimbali kwa Sisera kuwa nyara, mavazi ya rangi mbalimbali yaliyotariziwa, mavazi yaliyotariziwa vizuri kwa ajili ya shingo yangu: yote haya yakiwa nyara?’ 31“Adui zako wote na waangamie, Ee Bwana! Bali wote wakupendao na wawe kama jua lichomozavyo kwa nguvu zake.” Hivyo nchi ikawa na amani kwa miaka arobaini.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.