Waamuzi 5:16
Judges 5:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa nini ulikaa katikati ya mazizi ya kondoo kusikiliza sauti ya filimbi zinazoita makundi? Kwa jamaa za Reubeni, palikuwa na kujihoji kukubwa moyoni.
Judges 5:16 in English
Judges 5:16 · Berean Standard Bible
Why did you sit among the sheepfolds to hear the whistling for the flocks? In the clans of Reuben there was great indecision.
Context
14Kutoka Efraimu wakaja watu, ambao chimbuko lao ni Amaleki;
Benyamini akiwa miongoni
mwa watu waliokufuata.
Kutoka Makiri wakashuka viongozi,
na kutoka Zabuloni wale washikao
fimbo ya jemadari. 15Wakuu wa Isakari walikuwa pamoja na Debora;
naam, Isakari alikuwa pamoja na Baraka,
wakija nyuma yake kwa mbio
wakielekea bondeni.
Katika jamaa za Reubeni,
palikuwa na kujihoji kukubwa moyoni. 16Kwa nini ulikaa katikati ya mazizi ya kondoo
kusikiliza sauti ya filimbi zinazoita makundi?
Kwa jamaa za Reubeni,
palikuwa na kujihoji kukubwa moyoni. 17Gileadi alikaa ngʼambo ya Yordani.
Naye Dani, kwa nini alikaa
kwenye merikebu siku nyingi?
Asheri alikaa kwa utulivu ufuoni mwa bahari,
akikaa kwenye ghuba zake ndogo. 18Watu wa Zabuloni walihatarisha maisha yao,
vilevile nao watu wa Naftali.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.