Native Bible

Judges 3:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Basi Ehudi alikuwa ametengeneza upanga wenye ukatao kuwili, urefu wake ni kama dhiraa moja,* akaufunga upanga huo ndani ya nguo yake kwenye paja lake la mkono wa kuume.

Judges 3:16 in English

Judges 3:16 · Berean Standard Bible

Now Ehud had made for himself a double-edged sword a cubit long.* He strapped it to his right thigh under his cloak

Context

14Waisraeli wakawa chini ya Egloni mfalme wa Moabu kwa muda wa miaka kumi na minane. 15Waisraeli wakamlilia tena Bwana, naye akawapa mwokozi: Ehudi, mtu wa shoto, mwana wa Gera, Mbenyamini. Waisraeli wakatuma kwa Egloni mfalme wa Moabu ushuru kwa mkono wa Ehudi. 16Basi Ehudi alikuwa ametengeneza upanga wenye ukatao kuwili, urefu wake ni kama dhiraa moja,* akaufunga upanga huo ndani ya nguo yake kwenye paja lake la mkono wa kuume. 17Akamkabidhi ushuru Egloni mfalme wa Moabu, ambaye alikuwa mtu mnene sana. 18Baada ya Ehudi kumkabidhi ule ushuru, wale watu waliokuwa wameubeba huo ushuru aliwaruhusu waende zao.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.