Native Bible

Judges 3:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Waisraeli wakawa chini ya Egloni mfalme wa Moabu kwa muda wa miaka kumi na minane.

Judges 3:14 in English

Judges 3:14 · Berean Standard Bible

The Israelites served Eglon king of Moab eighteen years.

Context

12Waisraeli wakafanya maovu mbele za Bwana tena, kwa kuwa walifanya maovu hayo Bwana akamtia nguvu Egloni mfalme wa Moabu dhidi ya Israeli. 13Egloni akawataka Waamoni na Waamaleki waungane naye, akaja kuishambulia Israeli, nao wakatwaa Mji wa Mitende* 14Waisraeli wakawa chini ya Egloni mfalme wa Moabu kwa muda wa miaka kumi na minane. 15Waisraeli wakamlilia tena Bwana, naye akawapa mwokozi: Ehudi, mtu wa shoto, mwana wa Gera, Mbenyamini. Waisraeli wakatuma kwa Egloni mfalme wa Moabu ushuru kwa mkono wa Ehudi. 16Basi Ehudi alikuwa ametengeneza upanga wenye ukatao kuwili, urefu wake ni kama dhiraa moja,* akaufunga upanga huo ndani ya nguo yake kwenye paja lake la mkono wa kuume.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.