Waamuzi 2:21
Judges 2:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
mimi nami sitafukuza taifa lolote ambalo Yoshua aliliacha alipofariki.
Judges 2:21 in English
Judges 2:21 · Berean Standard Bible
I will no longer drive out before them any of the nations Joshua left when he died.
Context
19Lakini kila mara mwamuzi alipofariki, watu walirudia katika hali mbaya ya uovu zaidi kuliko baba zao, wakiifuata miungu mingine kuitumikia na kuiabudu. Walikataa kuacha matendo yao maovu na njia zao za ukaidi. 20Kwa hiyo Bwana akawakasirikia sana Israeli na kusema, “Kwa kuwa taifa hili limevunja Agano lile nililofanya na baba zao na hawakunisikiliza, 21mimi nami sitafukuza taifa lolote ambalo Yoshua aliliacha alipofariki. 22Nitayatumia ili nipate kuwapima Israeli na kuona kama wataishika njia ya Bwana na kuenenda katika hiyo kama njia baba zao walivyofanya.” 23Bwana alikuwa ameyaacha hayo mataifa yabaki; hakuyaondoa mara moja kwa kuyatia mikononi mwa Yoshua.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.