Waamuzi 17:2
Judges 17:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Akamwambia mama yake, “Zile shekeli 1,100* za fedha zilizochukuliwa kwako, ambazo nilisikia ukizinenea maneno ya laana, hizi hapa; mimi ndiye niliyezichukua, lakini sasa ninakurudishia.” Ndipo mama yake akamwambia, “Bwana na akubariki, mwanangu.”
Judges 17:2 in English
Judges 17:2 · Berean Standard Bible
said to his mother, “The eleven hundred shekels of silver * that were taken from you and about which I heard you utter a curse—I have the silver here with me; I took it.” Then his mother said, “Blessed be my son by the LORD!”
Context
1Palikuwa na mtu aliyeitwa Mika ambaye aliishi katika vilima vya Efraimu. 2Akamwambia mama yake, “Zile shekeli 1,100* za fedha zilizochukuliwa kwako, ambazo nilisikia ukizinenea maneno ya laana, hizi hapa; mimi ndiye niliyezichukua, lakini sasa ninakurudishia.”
Ndipo mama yake akamwambia, “Bwana na akubariki, mwanangu.” 3Alipozirudisha zile shekeli 1,100 za fedha kwa mama yake, mama yake akamwambia, “Mimi nimeiweka fedha hii wakfu kwa Bwana kwa ajili ya mwanangu kutengenezea kinyago cha kuchonga na sanamu ya kusubu. Mimi nitakurudishia wewe.” 4Hivyo akamrudishia mama yake ile fedha, naye mama yake akachukua shekeli mia mbili* za hiyo fedha na kumpa mfua fedha, ambaye aliifanyiza kinyago na sanamu. Navyo vikawekwa ndani ya nyumba ya Mika.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.