Waamuzi 17:1
Judges 17:1 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Palikuwa na mtu aliyeitwa Mika ambaye aliishi katika vilima vya Efraimu.
Judges 17:1 in English
Judges 17:1 · Berean Standard Bible
Now a man named Micah from the hill country of Ephraim
Context
1Palikuwa na mtu aliyeitwa Mika ambaye aliishi katika vilima vya Efraimu. 2Akamwambia mama yake, “Zile shekeli 1,100* za fedha zilizochukuliwa kwako, ambazo nilisikia ukizinenea maneno ya laana, hizi hapa; mimi ndiye niliyezichukua, lakini sasa ninakurudishia.”
Ndipo mama yake akamwambia, “Bwana na akubariki, mwanangu.” 3Alipozirudisha zile shekeli 1,100 za fedha kwa mama yake, mama yake akamwambia, “Mimi nimeiweka fedha hii wakfu kwa Bwana kwa ajili ya mwanangu kutengenezea kinyago cha kuchonga na sanamu ya kusubu. Mimi nitakurudishia wewe.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.