Native Bible

Judges 17:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hivyo akamrudishia mama yake ile fedha, naye mama yake akachukua shekeli mia mbili* za hiyo fedha na kumpa mfua fedha, ambaye aliifanyiza kinyago na sanamu. Navyo vikawekwa ndani ya nyumba ya Mika.

Judges 17:4 in English

Judges 17:4 · Berean Standard Bible

So he returned the silver to his mother, and she took two hundred shekels of silver * and gave them to a silversmith, who made them into a graven image and a molten idol. And they were placed in the house of Micah.

Context

2Akamwambia mama yake, “Zile shekeli 1,100* za fedha zilizochukuliwa kwako, ambazo nilisikia ukizinenea maneno ya laana, hizi hapa; mimi ndiye niliyezichukua, lakini sasa ninakurudishia.” Ndipo mama yake akamwambia, “Bwana na akubariki, mwanangu.” 3Alipozirudisha zile shekeli 1,100 za fedha kwa mama yake, mama yake akamwambia, “Mimi nimeiweka fedha hii wakfu kwa Bwana kwa ajili ya mwanangu kutengenezea kinyago cha kuchonga na sanamu ya kusubu. Mimi nitakurudishia wewe.” 4Hivyo akamrudishia mama yake ile fedha, naye mama yake akachukua shekeli mia mbili* za hiyo fedha na kumpa mfua fedha, ambaye aliifanyiza kinyago na sanamu. Navyo vikawekwa ndani ya nyumba ya Mika. 5Basi Mika alikuwa na mahali pa kuabudia miungu, akatengeneza naivera, pamoja na vinyago, na kumweka mmoja wa wanawe kuwa kuhani wake. 6Katika siku hizo Israeli hawakuwa na mfalme, kila mmoja akafanya kama alivyoona vyema machoni pake mwenyewe.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.