Waamuzi 14:12
Judges 14:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Samsoni akawaambia, “Niwape kitendawili, mkiweza kunipa jibu katika muda wa siku hizi saba za karamu, nitawapa mavazi thelathini ya kitani na mavazi mengine mivao thelathini.
Judges 14:12 in English
Judges 14:12 · Berean Standard Bible
“Let me tell you a riddle,” Samson said to them. “If you can solve it for me within the seven days of the feast, I will give you thirty linen garments and thirty sets of clothes.
Context
10Basi baba yake akateremka kumwona huyo mwanamke. Samsoni akafanya karamu huko, kama ilivyokuwa desturi ya vijana. 11Watu walipomwona, wakaleta vijana wenzake thelathini ili kuwa pamoja naye. 12Samsoni akawaambia, “Niwape kitendawili, mkiweza kunipa jibu katika muda wa siku hizi saba za karamu, nitawapa mavazi thelathini ya kitani na mavazi mengine mivao thelathini. 13Lakini msipoweza kufumbua, ndipo ninyi mtanipa mavazi thelathini ya kitani na mavazi mengine mivao thelathini.”
Wakamwambia, “Tuambie hicho kitendawili, hebu na tukisikie.” 14Akawaambia,
“Ndani ya mlaji,
kulitoka kitu cha kuliwa,
ndani ya mwenye nguvu,
kulitoka kitu kitamu.”
Kwa muda wa siku tatu hawakuweza kutoa jibu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.