Waamuzi 14:11
Judges 14:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Watu walipomwona, wakaleta vijana wenzake thelathini ili kuwa pamoja naye.
Judges 14:11 in English
Judges 14:11 · Berean Standard Bible
And when the Philistines saw him,* they selected thirty men to accompany him.
Context
9akachukua asali mkononi mwake akaendelea huku akila. Alipowafikia baba yake na mama yake, akawapa ile asali nao wakala. Lakini hakuwaambia kuwa alitwaa asali kutoka kwenye mzoga wa simba. 10Basi baba yake akateremka kumwona huyo mwanamke. Samsoni akafanya karamu huko, kama ilivyokuwa desturi ya vijana. 11Watu walipomwona, wakaleta vijana wenzake thelathini ili kuwa pamoja naye. 12Samsoni akawaambia, “Niwape kitendawili, mkiweza kunipa jibu katika muda wa siku hizi saba za karamu, nitawapa mavazi thelathini ya kitani na mavazi mengine mivao thelathini. 13Lakini msipoweza kufumbua, ndipo ninyi mtanipa mavazi thelathini ya kitani na mavazi mengine mivao thelathini.”
Wakamwambia, “Tuambie hicho kitendawili, hebu na tukisikie.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.