Native Bible

Judges 13:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Basi Manoa akamuuliza, “Wakati maneno yako yatakapotimia, masharti ya maisha ya mtoto huyu yatakuwa nini na kazi yake itakuwa ni nini?”

Judges 13:12 in English

Judges 13:12 · Berean Standard Bible

Then Manoah asked, “When your words come to pass, what will be the boy’s rule of life and mission?”

Context

10Basi yule mwanamke akaenda haraka na kumwambia mumewe, “Tazama mtu yule aliyenitokea siku ile yupo hapa!” 11Manoa akainuka akaandamana na mkewe. Alipomfikia yule mtu akamuuliza, “Je, wewe ndiye yule uliyesema na mke wangu?” Akasema, “Mimi ndiye.” 12Basi Manoa akamuuliza, “Wakati maneno yako yatakapotimia, masharti ya maisha ya mtoto huyu yatakuwa nini na kazi yake itakuwa ni nini?” 13Malaika wa Bwana akamjibu, “Mke wako hana budi kufanya yale yote niliyomwambia. 14Kamwe asile kitu chochote kitakachotoka katika mzabibu, wala asinywe mvinyo wa aina yoyote wala kileo chochote wala asile kitu chochote kilicho najisi. Hana budi kufanya kila kitu nilichomwagiza.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.