Native Bible

James 1:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Lakini anapoomba, lazima aamini wala asiwe na shaka, kwa sababu mtu aliye na shaka ni kama wimbi la bahari, lililochukuliwa na upepo na kutupwa huku na huku.

James 1:6 in English

James 1:6 · Berean Standard Bible

But he must ask in faith, without doubting, because he who doubts is like a wave of the sea, blown and tossed by the wind.

Context

4Saburi na iwe na kazi timilifu, ili mpate kuwa wakamilifu, mmekamilishwa, bila kupungukiwa na kitu chochote. 5Kama mtu yeyote miongoni mwenu amepungukiwa na hekima na amwombe Mungu, yeye awapaye watu wote kwa ukarimu wala hana kinyongo, naye atapewa. 6Lakini anapoomba, lazima aamini wala asiwe na shaka, kwa sababu mtu aliye na shaka ni kama wimbi la bahari, lililochukuliwa na upepo na kutupwa huku na huku. 7Mtu kama huyo asidhani ya kuwa atapata kitu chochote kutoka kwa Bwana. 8Yeye ni mtu mwenye nia mbili, mwenye kusitasita katika njia zake zote.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.