Isaya 9:14
Isaiah 9:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa hiyo Bwana atakatilia mbali kutoka Israeli kichwa na mkia, tawi la mtende na tete katika siku moja.
Isaiah 9:14 in English
Isaiah 9:14 · Berean Standard Bible
So the LORD will cut off Israel’s head and tail, both palm branch and reed in a single day.
Context
12Waashuru kutoka upande wa mashariki
na Wafilisti kutoka upande wa magharibi
wameila Israeli kwa kinywa kilichopanuliwa.
Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali,
mkono wake bado umeinuliwa juu. 13Lakini watu hawajamrudia yeye aliyewapiga,
wala hawajamtafuta Bwana Mwenye Nguvu Zote. 14Kwa hiyo Bwana atakatilia mbali kutoka Israeli kichwa na mkia,
tawi la mtende na tete katika siku moja. 15Wazee na watu mashuhuri ndio vichwa,
nao manabii wanaofundisha uongo ndio mkia. 16Wale wanaowaongoza watu hawa wanawapotosha,
nao wale wanaoongozwa wamepotoka.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.