Isaya 7:8
Isaiah 7:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
kwa kuwa kichwa cha Aramu ni Dameski, na kichwa cha Dameski ni Resini peke yake. Katika muda wa miaka sitini na mitano, Efraimu atakuwa ameharibiwa kiasi kwamba hataweza tena kuwa taifa.
Isaiah 7:8 in English
Isaiah 7:8 · Berean Standard Bible
For the head of Aram is Damascus, and the head of Damascus is Rezin. Within sixty-five years Ephraim will be shattered as a people.
Context
6“Tuishambulie Yuda, naam, tuirarue vipande vipande na kuigawa miongoni mwetu, na kumtawaza mwana wa Tabeeli awe mfalme juu yake.” 7Lakini Bwana Mwenyezi asema hivi:
“ ‘Jambo hili halitatendeka,
halitatokea, 8kwa kuwa kichwa cha Aramu ni Dameski,
na kichwa cha Dameski ni Resini peke yake.
Katika muda wa miaka sitini na mitano,
Efraimu atakuwa ameharibiwa
kiasi kwamba hataweza tena kuwa taifa. 9Kichwa cha Efraimu ni Samaria,
na kichwa cha Samaria
ni mwana wa Remalia peke yake.
Kama hamtasimama thabiti katika imani yenu,
hamtaimarika kamwe.’ ” 10Bwana akasema na Ahazi tena,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.