Isaya 7:15
Isaiah 7:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Atakula jibini na asali atakapokuwa ameweza kukataa mabaya na kuchagua mema.
Isaiah 7:15 in English
Isaiah 7:15 · Berean Standard Bible
By the time He knows enough to reject evil and choose good, He will be eating curds and honey.
Context
13Ndipo Isaya akasema, “Sikia sasa, ewe nyumba ya Daudi! Je, haitoshi kujaribu uvumilivu wa wanadamu? Je, mtaujaribu uvumilivu wa Mungu wangu pia? 14Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara: Bikira atachukua mimba, naye atamzaa mwana, na ataitwa Imanueli.* 15Atakula jibini na asali atakapokuwa ameweza kukataa mabaya na kuchagua mema. 16Lakini kabla mtoto hajajua kukataa mabaya na kuchagua mema, nchi ya wafalme hao wawili unaowaogopa itafanywa ukiwa. 17Bwana ataleta juu yako, juu ya watu wako, na juu ya nyumba ya baba yako wakati ambao haujawahi kuwako tangu Efraimu alipojitenga na Yuda: yeye atawaleteeni mfalme wa Ashuru.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.