Isaya 66:7
Isaiah 66:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Kabla hajasikia utungu, alizaa; kabla hajapata maumivu, alizaa mtoto mwanaume.
Isaiah 66:7 in English
Isaiah 66:7 · Berean Standard Bible
“Before she was in labor, she gave birth; before she was in pain, she delivered a boy.
Context
5Sikieni neno la Bwana,
ninyi mtetemekao kwa neno lake:
“Ndugu zenu wanaowachukia ninyi
na kuwatenga ninyi kwa sababu ya Jina langu, wamesema,
‘Bwana na atukuzwe,
ili tupate kuona furaha yenu!’
Hata sasa wataaibika. 6Sikieni hizo ghasia kutoka mjini,
sikieni hizo kelele kutoka hekaluni!
Ni sauti ya Bwana ikiwalipa adui zake
yote wanayostahili. 7“Kabla hajasikia utungu, alizaa;
kabla hajapata maumivu,
alizaa mtoto mwanaume. 8Ni nani amepata kusikia jambo kama hili?
Ni nani amepata kuona mambo kama haya?
Je, nchi yaweza kuzaliwa kwa siku moja,
au taifa laweza kutokea mara?
Mara Sayuni alipoona utungu,
alizaa watoto wake. 9Je, nilete mwana hadi wakati wa kuzaliwa
na nisizalishe?” asema Bwana.
“Je, nifunge tumbo la uzazi
wakati mimi ndiye nizalishaye?”
asema Mungu wako.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.