Native Bible

Isaiah 65:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kabla hawajaita, nitajibu, nao wakiwa katika kunena, nitasikia.

Isaiah 65:24 in English

Isaiah 65:24 · Berean Standard Bible

Even before they call, I will answer, and while they are still speaking, I will hear.

Context

22Hawatajenga nyumba, nao watu wengine waishi ndani yake, au kupanda mazao na wengine wale. Kwa kuwa kama zilivyo siku za mti, ndivyo zitakavyokuwa siku za watu wangu, wateule wangu watafurahia kwa siku nyingi kazi za mikono yao. 23Hawatajitaabisha kwa kazi bure, wala hawatazaa watoto ili wapatwe na majanga, kwa kuwa watakuwa taifa lililobarikiwa na Bwana, wao na wazao wao pamoja nao. 24Kabla hawajaita, nitajibu, nao wakiwa katika kunena, nitasikia. 25Mbwa mwitu na mwana-kondoo watalisha pamoja, naye simba atakula nyasi kama maksai, lakini mavumbi yatakuwa chakula cha nyoka. Hawatadhuru wala kuharibu katika mlima wangu mtakatifu wote,” asema Bwana.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.