Isaya 65:17
Isaiah 65:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Tazama, nitaumba mbingu mpya na dunia mpya. Mambo ya zamani hayatakumbukwa, wala hayatakuja akilini.
Isaiah 65:17 in English
Isaiah 65:17 · Berean Standard Bible
For behold, I will create new heavens and a new earth.* The former things will not be remembered, nor will they come to mind.
Context
15Mtaliacha jina lenu
kuwa laana kwa watu wangu waliochaguliwa;
Bwana Mwenyezi atawaua ninyi,
lakini watumishi wake atawapa jina jingine. 16Yeye aombaye baraka katika nchi
atafanya hivyo kwa Mungu wa kweli;
yeye aapaye katika nchi
ataapa kwa Mungu wa kweli.
Kwa kuwa taabu za zamani zitasahaulika
na kufichwa kutoka machoni pangu. 17“Tazama, nitaumba
mbingu mpya na dunia mpya.
Mambo ya zamani hayatakumbukwa,
wala hayatakuja akilini. 18Lakini furahini na kushangilia daima
katika hivi nitakavyoumba,
kwa kuwa nitaumba Yerusalemu uwe wa kupendeza,
nao watu wake wawe furaha. 19Nami nitaifurahia Yerusalemu
na kuwafurahia watu wangu;
sauti ya maombolezo na ya kilio
haitasikika humo tena.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.