Isaya 63:8
Isaiah 63:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Alisema, “Hakika wao ni watu wangu, wana ambao hawatanidanganya”; hivyo akawa Mwokozi wao.
Isaiah 63:8 in English
Isaiah 63:8 · Berean Standard Bible
For He said, “They are surely My people, sons who will not be disloyal.” So He became their Savior.
Context
6Nilikanyaga mataifa kwa miguu katika hasira yangu,
katika ghadhabu yangu niliwalewesha,
na kumwaga damu yao juu ya ardhi.” 7Nitasimulia juu ya wema wa Bwana,
kwa matendo ambayo apaswa kusifiwa,
sawasawa na yote ambayo Bwana
ametenda kwa ajili yetu:
naam, mambo mengi mema aliyoyatenda
kwa ajili ya nyumba ya Israeli,
sawasawa na huruma zake
na wema wake mwingi. 8Alisema, “Hakika wao ni watu wangu,
wana ambao hawatanidanganya”;
hivyo akawa Mwokozi wao. 9Katika taabu zao zote naye alitaabika,
na malaika wa uso wake akawaokoa.
Katika upendo wake na rehema zake aliwakomboa,
akawainua na kuwachukua siku zote zilizopita. 10Lakini waliasi,
na kumhuzunisha Roho Mtakatifu wake.
Hivyo aligeuka na kuwa adui yao,
na yeye mwenyewe akapigana dhidi yao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.