Isaya 59:8
Isaiah 59:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hawajui njia ya amani, hakuna haki katika mapito yao. Wameyageuza kuwa njia za upotovu, hakuna apitaye njia hizo atakayeifahamu amani.
Isaiah 59:8 in English
Isaiah 59:8 · Berean Standard Bible
The way of peace they have not known,* and there is no justice in their tracks. They have turned them into crooked paths; no one who treads on them will know peace.
Context
6Utando wao wa buibui haufai kwa nguo;
hawawezi kujifunika kwa kile walichokitengeneza.
Matendo yao ni matendo maovu,
vitendo vya jeuri vipo mikononi mwao. 7Miguu yao hukimbilia kwenye dhambi,
ni myepesi kumwaga damu isiyo na hatia.
Mawazo yao ni mawazo maovu;
uharibifu na maangamizi huonekana katika njia zao. 8Hawajui njia ya amani,
hakuna haki katika mapito yao.
Wameyageuza kuwa njia za upotovu,
hakuna apitaye njia hizo atakayeifahamu amani. 9Hivyo uadilifu uko mbali nasi,
nayo haki haitufikii.
Tunatazamia nuru, kumbe! Yote ni giza,
tunatazamia mwanga, lakini tunatembea katika giza kuu. 10Tunapapasa ukuta kama kipofu,
tunapapasa katika njia zetu kama watu wasio na macho.
Adhuhuri tunajikwaa kama wakati wa gizagiza;
katikati ya wenye nguvu, tuko kama wafu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.