Isaya 59:17
Isaiah 59:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Alivaa haki kama dirii kifuani mwake, na chapeo ya wokovu kichwani mwake, alivaa mavazi ya kisasi naye akajifunga wivu kama joho.
Isaiah 59:17 in English
Isaiah 59:17 · Berean Standard Bible
He put on righteousness like a breastplate, and the helmet of salvation on His head; He put on garments of vengeance and wrapped Himself in a cloak of zeal.
Context
15Kweli haipatikani popote,
na yeyote aepukaye uovu huwa mawindo.
Bwana alitazama naye akachukizwa
kwamba hapakuwepo haki. 16Aliona kuwa hakuwepo hata mtu mmoja,
akashangaa kwamba hakuwepo hata mmoja wa kuingilia kati;
hivyo mkono wake mwenyewe
ndio uliomfanyia wokovu,
nayo haki yake mwenyewe
ndiyo iliyomtegemeza. 17Alivaa haki kama dirii kifuani mwake,
na chapeo ya wokovu kichwani mwake,
alivaa mavazi ya kisasi
naye akajifunga wivu kama joho. 18Kulingana na kile walichokuwa wametenda,
ndivyo atakavyolipa
ghadhabu kwa watesi wake
na kisasi kwa adui zake,
atavilipa visiwa sawa na wanavyostahili. 19Kuanzia magharibi, watu wataliogopa jina la Bwana
na kuanzia mawio ya jua, watauheshimu utukufu wake.
Wakati adui atakapokuja kama mafuriko,
Roho wa Bwana atainua kiwango dhidi yake na kumshinda.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.