Isaya 58:10
Isaiah 58:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
nanyi kama mkimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi zenu na kutosheleza mahitaji ya walioonewa, ndipo nuru yenu itakapongʼaa gizani, nao usiku wenu utakuwa kama adhuhuri.
Isaiah 58:10 in English
Isaiah 58:10 · Berean Standard Bible
and if you give yourself to the hungry and satisfy the afflicted soul, then your light will go forth in the darkness, and your night will be like noonday.
Context
8Ndipo nuru yako itajitokeza kama mapambazuko
na uponyaji wako utatokea upesi;
ndipo haki yako itakapokutangulia mbele yako,
na utukufu wa Bwana utakuwa mlinzi nyuma yako. 9Ndipo utaita, naye Bwana atajibu,
utalia kuomba msaada,
naye atasema: Mimi hapa.
“Kama ukiiondoa nira ya udhalimu,
na kunyoosha kidole na kuzungumza maovu, 10nanyi kama mkimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi zenu
na kutosheleza mahitaji ya walioonewa,
ndipo nuru yenu itakapongʼaa gizani,
nao usiku wenu utakuwa kama adhuhuri. 11Bwana atakuongoza siku zote,
atayatosheleza mahitaji yako katika nchi kame,
naye ataitia nguvu mifupa yako.
Utakuwa kama bustani iliyonyweshwa vizuri,
kama chemchemi ambayo maji yake hayakauki kamwe. 12Watu wako watajenga tena magofu ya zamani
na kuinua misingi ya kale;
utaitwa Mwenye Kukarabati Kuta Zilizobomoka,
Mwenye Kurejeza Barabara za Makao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.