Isaya 58:12
Isaiah 58:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Watu wako watajenga tena magofu ya zamani na kuinua misingi ya kale; utaitwa Mwenye Kukarabati Kuta Zilizobomoka, Mwenye Kurejeza Barabara za Makao.
Isaiah 58:12 in English
Isaiah 58:12 · Berean Standard Bible
Your people will rebuild the ancient ruins; you will restore the age-old foundations; you will be called Repairer of the Breach, Restorer of the Streets of Dwelling.
Context
10nanyi kama mkimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi zenu
na kutosheleza mahitaji ya walioonewa,
ndipo nuru yenu itakapongʼaa gizani,
nao usiku wenu utakuwa kama adhuhuri. 11Bwana atakuongoza siku zote,
atayatosheleza mahitaji yako katika nchi kame,
naye ataitia nguvu mifupa yako.
Utakuwa kama bustani iliyonyweshwa vizuri,
kama chemchemi ambayo maji yake hayakauki kamwe. 12Watu wako watajenga tena magofu ya zamani
na kuinua misingi ya kale;
utaitwa Mwenye Kukarabati Kuta Zilizobomoka,
Mwenye Kurejeza Barabara za Makao. 13“Kama ukitunza miguu yako isivunje Sabato,
na kutokufanya kama vile upendavyo katika siku yangu takatifu,
kama ukiita Sabato siku ya furaha
na siku takatifu ya Bwana ya kuheshimiwa,
kama utaiheshimu kwa kutoenenda
katika njia zako mwenyewe,
na kutokufanya yakupendezayo
au kusema maneno ya upuzi, 14ndipo utakapojipatia furaha yako katika Bwana,
nami nitakufanya upande juu ya miinuko ya nchi
na kusherehekea urithi wa Yakobo baba yako.”
Kinywa cha Bwana kimenena haya.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.