Isaya 57:18
Isaiah 57:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nimeziona njia zake, lakini nitamponya, nitamwongoza na kumrudishia upya faraja,
Isaiah 57:18 in English
Isaiah 57:18 · Berean Standard Bible
I have seen his ways, but I will heal him; I will guide him and restore comfort to him and his mourners,
Context
16Sitaendelea kulaumu milele,
wala sitakasirika siku zote,
kwa kuwa roho ya mwanadamu
ingezimia mbele zangu:
yaani pumzi ya mwanadamu niliyemuumba. 17Nilighadhibika na tamaa yake ya dhambi;
nilimwadhibu, nikauficha uso wangu kwa hasira,
na bado aliendelea katika njia zake za tamaa. 18Nimeziona njia zake, lakini nitamponya,
nitamwongoza na kumrudishia upya faraja, 19nikiumba sifa midomoni ya waombolezaji
katika Israeli.
Amani, amani, kwa wale walio mbali
na kwa wale walio karibu,”
asema Bwana. “Nami nitawaponya.” 20Bali waovu ni kama bahari ichafukayo,
ambayo haiwezi kutulia,
mawimbi yake hutupa takataka na matope.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.