Isaya 54:7
Isaiah 54:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Kwa kitambo kidogo nilikuacha, lakini kwa huruma nyingi nitakurudisha.
Isaiah 54:7 in English
Isaiah 54:7 · Berean Standard Bible
“For a brief moment I forsook you, but with great compassion I will bring you back.
Context
5Kwa maana Muumba wako ndiye mume wako,
Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake,
yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli ni Mkombozi wako,
yeye anaitwa Mungu wa dunia yote. 6Bwana atakuita urudi
kana kwamba ulikuwa mke aliyeachwa na kuhuzunishwa rohoni;
kama mke aliyeolewa bado angali kijana
na kukataliwa,” asema Mungu wako. 7“Kwa kitambo kidogo nilikuacha,
lakini kwa huruma nyingi nitakurudisha. 8Katika ukali wa hasira
nilikuficha uso wangu kwa kitambo,
lakini kwa fadhili za milele
nitakuwa na huruma juu yako,”
asema Bwana Mkombozi wako. 9“Kwangu mimi jambo hili ni kama siku za Noa,
nilipoapa kuwa maji ya Noa kamwe hayatafunika tena dunia.
Hivyo sasa nimeapa sitawakasirikia ninyi,
kamwe sitawakemea tena.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.