Isaya 53:1
Isaiah 53:1 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ni nani aliyeamini ujumbe wetu, na mkono wa Bwana umefunuliwa kwa nani?
Isaiah 53:1 in English
Isaiah 53:1 · Berean Standard Bible
Who has believed our message? And to whom has the arm of the LORD been revealed?*
Context
1Ni nani aliyeamini ujumbe wetu,
na mkono wa Bwana umefunuliwa kwa nani? 2Alikua mbele yake kama mche mwororo
na kama mzizi katika nchi kavu.
Hakuwa na uzuri wala utukufu wa kutuvutia kwake,
hakuwa na chochote katika sura yake cha kutufanya tumtamani. 3Alidharauliwa na kukataliwa na wanadamu,
mtu wa huzuni nyingi, ajuaye mateso.
Kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao,
alidharauliwa, wala hatukumhesabu kuwa kitu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.