Isaya 51:15
Isaiah 51:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa maana Mimi ndimi Bwana, Mungu wako, ambaye huisukasuka bahari ili mawimbi yake yangurume: Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake.
Isaiah 51:15 in English
Isaiah 51:15 · Berean Standard Bible
For I am the LORD your God who stirs up the sea so that its waves roar— the LORD of Hosts is His name.
Context
13kwamba mnamsahau Bwana Muumba wenu,
aliyezitanda mbingu
na kuiweka misingi ya dunia,
kwamba mnaishi katika hofu siku zote
kwa sababu ya ghadhabu ya mdhalimu,
ambaye nia yake ni kuangamiza?
Iko wapi basi ghadhabu ya mdhalimu? 14Wafungwa waliojikunyata kwa hofu
watawekwa huru karibuni;
hawatafia kwenye gereza lao,
wala hawatakosa chakula. 15Kwa maana Mimi ndimi Bwana, Mungu wako,
ambaye huisukasuka bahari ili mawimbi yake yangurume:
Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake. 16Nimeweka maneno yangu kinywani mwako
na kukufunika kwa uvuli wa mkono wangu:
Mimi niliyeweka mbingu mahali pake,
niliyeweka misingi ya dunia,
niwaambiaye Sayuni,
‘Ninyi ni watu wangu.’ ” 17Amka, amka!
Simama, ee Yerusalemu,
wewe uliyekunywa kutoka mkono wa Bwana
kikombe cha ghadhabu yake,
wewe uliyekunywa mpaka kufikia machujo yake,
kikombe kile cha kunywea
kiwafanyacho watu kuyumbayumba.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.