Isaya 51:1
Isaiah 51:1 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Nisikilizeni, ninyi mnaofuatia haki na mnaomtafuta Bwana: Tazameni mwamba ambako mlichongwa, na mahali pa kuvunjia mawe ambako mlichimbwa;
Isaiah 51:1 in English
Isaiah 51:1 · Berean Standard Bible
“Listen to Me, you who pursue righteousness, you who seek the LORD: Look to the rock from which you were cut, and to the quarry from which you were hewn.
Context
1“Nisikilizeni, ninyi mnaofuatia haki
na mnaomtafuta Bwana:
Tazameni mwamba ambako mlichongwa,
na mahali pa kuvunjia mawe ambako mlichimbwa; 2mwangalieni Abrahamu, baba yenu,
na Sara, ambaye aliwazaa.
Wakati nilipomwita alikuwa mmoja tu,
nami nikambariki na kumfanya kuwa wengi. 3Hakika Bwana ataifariji Sayuni,
naye atayaangalia kwa huruma magofu yake yote;
atayafanya majangwa yake yawe kama Edeni,
nazo sehemu zake zisizolimika ziwe kama bustani ya Bwana.
Shangwe na furaha zitakuwako ndani yake,
shukrani na sauti za kuimba.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.