Isaya 50:4
Isaiah 50:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Bwana Mwenyezi amenipa ulimi uliofundishwa, ili kujua neno limtegemezalo aliyechoka. Huniamsha asubuhi kwa asubuhi, huamsha sikio langu lisikie kama mtu afundishwaye.
Isaiah 50:4 in English
Isaiah 50:4 · Berean Standard Bible
The Lord GOD has given Me the tongue of discipleship, to sustain the weary with a word. He awakens Me morning by morning; He awakens My ear to listen as a disciple.
Context
2Nilipokuja, kwa nini hakuwepo hata mmoja?
Nilipoita, kwa nini hakuwepo hata mmoja wa kujibu?
Je, mkono wangu ni mfupi mno hata nisiweze kuwakomboa?
Je, mimi sina nguvu za kukuokoa?
Kwa kukemea tu naikausha bahari,
naigeuza mito ya maji kuwa jangwa;
samaki wake wanaoza kwa kukosa maji
na kufa kwa ajili ya kiu. 3Ninalivika anga weusi na kufanya nguo ya gunia
kuwa kifuniko chake.” 4Bwana Mwenyezi amenipa ulimi uliofundishwa,
ili kujua neno limtegemezalo aliyechoka.
Huniamsha asubuhi kwa asubuhi,
huamsha sikio langu lisikie kama mtu afundishwaye. 5Bwana Mwenyezi amezibua masikio yangu,
nami sikuwa mwasi,
wala sikurudi nyuma. 6Niliwapa mgongo wangu wale wanipigao,
mashavu yangu wale wangʼoao ndevu zangu;
sikuuficha uso wangu kutokana na fedheha
na kutemewa mate.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.