Isaya 5:14
Isaiah 5:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa hiyo kaburi* limeongeza hamu yake na kupanua mdomo wake bila kikomo, ndani mwake watashuka wakuu wao na wingi wa watu, pamoja na wagomvi wao, na wafanyao sherehe wote.
Isaiah 5:14 in English
Isaiah 5:14 · Berean Standard Bible
Therefore Sheol enlarges its throat and opens wide its enormous jaws, and down go Zion’s nobles and masses, her revelers and carousers!
Context
12Wana vinubi na zeze kwenye karamu zao,
matari, filimbi na mvinyo,
lakini hawayajali matendo ya Bwana,
wala hawana heshima kwa ajili ya kazi ya mikono yake. 13Kwa hiyo watu wangu watakwenda uhamishoni
kwa sababu ya kukosa ufahamu,
watu wao wenye vyeo watakufa kwa njaa
na watu wao wengi watakauka kwa kiu. 14Kwa hiyo kaburi* limeongeza hamu yake
na kupanua mdomo wake bila kikomo,
ndani mwake watashuka wakuu wao na wingi wa watu,
pamoja na wagomvi wao, na wafanyao sherehe wote. 15Hivyo mwanadamu atashushwa,
na binadamu kunyenyekezwa,
macho ya wenye majivuno yatanyenyekezwa. 16Lakini Bwana Mwenye Nguvu Zote atatukuzwa
kwa ajili ya haki yake,
naye Mungu Mtakatifu atajionyesha mwenyewe
kuwa mtakatifu kwa haki yake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.