Isaya 48:19
Isaiah 48:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wazao wako wangekuwa kama mchanga, watoto wako kama chembe zake zisizohesabika; kamwe jina lao lisingefutiliwa mbali, wala kuangamizwa kutoka mbele zangu.”
Isaiah 48:19 in English
Isaiah 48:19 · Berean Standard Bible
Your descendants would have been as countless as the sand, and your offspring as numerous as its grains;* their name would never be cut off or eliminated from My presence.”
Context
17Hili ndilo asemalo Bwana,
Mkombozi wako, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli:
“Mimi ni Bwana, Mungu wako,
nikufundishaye ili upate faida,
nikuongozaye katika njia ikupasayo kuiendea. 18Laiti ungesikiliza kwa makini maagizo yangu,
amani yako ingekuwa kama mto,
haki yako kama mawimbi ya bahari. 19Wazao wako wangekuwa kama mchanga,
watoto wako kama chembe zake zisizohesabika;
kamwe jina lao lisingefutiliwa mbali,
wala kuangamizwa kutoka mbele zangu.” 20Tokeni huko Babeli,
kimbieni kutoka kwa Wakaldayo!
Tangazeni hili kwa kelele za shangwe
na kulihubiri.
Lipelekeni mpaka miisho ya dunia;
semeni, “Bwana amemkomboa
mtumishi wake Yakobo.” 21Hawakuona kiu alipowaongoza kupita jangwani;
alifanya maji yatiririke kutoka kwenye mwamba kwa ajili yao;
akapasua mwamba
na maji yakatoka kwa nguvu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.