Isaya 45:4
Isaiah 45:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa ajili ya Yakobo mtumishi wangu, Israeli niliyemchagua, nimekuita wewe kwa jina lako, na kukupa jina la heshima, ingawa wewe hunitambui.
Isaiah 45:4 in English
Isaiah 45:4 · Berean Standard Bible
For the sake of Jacob My servant and Israel My chosen one, I call you by name; I have given you a title of honor, though you have not known Me.
Context
2Nitakwenda mbele yako
na kusawazisha milima;
nitavunjavunja malango ya shaba
na kukatakata mapingo ya chuma. 3Nitakupa hazina za gizani,
mali zilizofichwa mahali pa siri,
ili upate kujua ya kwamba Mimi ndimi Bwana,
Mungu wa Israeli, akuitaye kwa jina lako. 4Kwa ajili ya Yakobo mtumishi wangu,
Israeli niliyemchagua,
nimekuita wewe kwa jina lako,
na kukupa jina la heshima,
ingawa wewe hunitambui. 5Mimi ndimi Bwana, wala hakuna mwingine,
zaidi yangu hakuna Mungu.
Nitakutia nguvu,
ingawa wewe hujanitambua, 6ili kutoka mawio ya jua
mpaka machweo yake,
watu wapate kujua kwamba hakuna Mungu mwingine ila Mimi.
Mimi ndimi Bwana wala hakuna mwingine.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.