Isaya 44:4
Isaiah 44:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nao watachipua kama manyasi katika shamba la majani, kama mierezi kando ya vijito vya maji yatiririkayo.
Isaiah 44:4 in English
Isaiah 44:4 · Berean Standard Bible
They will sprout among the grass like willows * by flowing streams.
Context
2Hili ndilo asemalo Bwana,
yeye aliyekuhuluku, aliyekuumba tumboni,
yeye atakayekusaidia:
Usiogope, ee Yakobo, mtumishi wangu,
Yeshuruni,* niliyekuchagua. 3Kwa maana nitamimina maji juu ya nchi yenye kiu,
na vijito vya maji juu ya ardhi iliyokauka;
nitamimina Roho wangu juu ya watoto wako,
nayo baraka yangu juu ya wazao wako. 4Nao watachipua kama manyasi katika shamba la majani,
kama mierezi kando ya vijito vya maji yatiririkayo. 5Mmoja atasema, ‘Mimi ni wa Bwana’;
mwingine atajiita kwa jina la Yakobo;
vilevile mwingine ataandika juu ya mkono wake, ‘Wa Bwana,’
na kujiita kwa jina la Israeli. 6“Hili ndilo asemalo Bwana,
Mfalme wa Israeli na Mkombozi,
Bwana Mwenye Nguvu Zote:
Mimi ni wa kwanza na Mimi ni wa mwisho;
zaidi yangu hakuna Mungu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.