Isaya 44:25
Isaiah 44:25 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“mimi huzipinga ishara za manabii wa uongo, na kuwatia upumbavu waaguzi, niyapinduaye maarifa ya wenye hekima, na kuyafanya kuwa upuzi,
Isaiah 44:25 in English
Isaiah 44:25 · Berean Standard Bible
who foils the signs of false prophets and makes fools of diviners, who confounds the wise and turns their knowledge into nonsense,
Context
23Enyi mbingu, imbeni kwa furaha,
kwa maana Bwana amefanya jambo hili.
Ee vilindi vya dunia, piga kelele.
Enyi milima, pazeni sauti kwa nyimbo,
enyi misitu na miti yenu yote,
kwa maana Bwana amemkomboa Yakobo,
ameuonyesha utukufu wake katika Israeli. 24“Hili ndilo asemalo Bwana,
Mkombozi wako, aliyekuumba tumboni:
“Mimi ni Bwana,
niliyeumba vitu vyote,
niliyezitanda mbingu peke yangu,
niliyeitandaza nchi mwenyewe, 25“mimi huzipinga ishara za manabii wa uongo,
na kuwatia upumbavu waaguzi,
niyapinduaye maarifa ya wenye hekima,
na kuyafanya kuwa upuzi, 26niyathibitishaye maneno ya watumishi wake,
na kutimiza utabiri wa wajumbe wake,
“niambiaye Yerusalemu, ‘Itakaliwa na watu,’
niambiaye miji ya Yuda kuwa, ‘Itajengwa,’
na kuhusu magofu yake, ‘Mimi nitayatengeneza,’ 27niambiaye kilindi cha maji, ‘Kauka,
nami nitakausha vijito vyako,’
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.