Native Bible

Isaiah 43:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Uwaongoze wale wenye macho lakini hawaoni, wenye masikio lakini hawasikii.

Isaiah 43:8 in English

Isaiah 43:8 · Berean Standard Bible

Bring out a people who have eyes but are blind, and who have ears but are deaf.

Context

6Nitaiambia kaskazini, ‘Watoe!’ nayo kusini, ‘Usiwazuie.’ Walete wana wangu kutoka mbali, na binti zangu kutoka miisho ya dunia: 7kila mmoja ambaye ameitwa kwa Jina langu, niliyemuumba kwa utukufu wangu, niliyemhuluku na kumfanya.” 8Uwaongoze wale wenye macho lakini hawaoni, wenye masikio lakini hawasikii. 9Mataifa yote yanakutanika pamoja, na makabila yanakusanyika. Ni nani miongoni mwao aliyetangulia kutuambia haya, na kututangazia mambo yaliyopita? Walete mashahidi wao ili kuwathibitisha kuwa walikuwa sahihi, ili wengine waweze kusikia, waseme, “Ni kweli.” 10“Ninyi ni mashahidi wangu,” asema Bwana, “na mtumishi wangu niliyemchagua, ili mpate kunijua na kuniamini, na kutambua kwamba Mimi ndiye. Kabla yangu hakuna mungu aliyefanyizwa, wala hatakuwepo mwingine baada yangu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.