Isaya 43:7
Isaiah 43:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
kila mmoja ambaye ameitwa kwa Jina langu, niliyemuumba kwa utukufu wangu, niliyemhuluku na kumfanya.”
Isaiah 43:7 in English
Isaiah 43:7 · Berean Standard Bible
everyone called by My name and created for My glory, whom I have indeed formed and made.”
Context
5Usiogope, kwa kuwa mimi nipo pamoja nawe,
nitawaleta watoto wako kutoka mashariki,
na kukukusanya kutoka magharibi. 6Nitaiambia kaskazini, ‘Watoe!’
nayo kusini, ‘Usiwazuie.’
Walete wana wangu kutoka mbali,
na binti zangu kutoka miisho ya dunia: 7kila mmoja ambaye ameitwa kwa Jina langu,
niliyemuumba kwa utukufu wangu,
niliyemhuluku na kumfanya.” 8Uwaongoze wale wenye macho lakini hawaoni,
wenye masikio lakini hawasikii. 9Mataifa yote yanakutanika pamoja,
na makabila yanakusanyika.
Ni nani miongoni mwao aliyetangulia kutuambia haya,
na kututangazia mambo yaliyopita?
Walete mashahidi wao ili kuwathibitisha kuwa walikuwa sahihi,
ili wengine waweze kusikia, waseme, “Ni kweli.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.